MATOKEO YA DARAJA LA PILI KITAIFA, FURUNZI YACHEMKA ALASKAN

Klabu ya Yanga inayoongopzwa na mkufunzi Collins Omol iliitandika Furunzi Fc ya Mkufunzi Nero Chishenga kichapo cha mabao 4-1 katika derby ya kaunti ya kilifi.

Ni mechi ambayo ilishuhudia kadi tatu nyuekundu zikitenbea kwa wachezaji huku Furunzi FC ikipokea mbili na Yanga Kadi moja ukiwa ni mchezo wa pili wawili hawa wanakutana ikizingatiwa kwamba katika raundi ya kwanza Uwanjani Alaskan Furunzi wakiwa nyumbani walilazimishwa sare ya vijana hao wa Yanga.

Simba apparel waliwalazimisha Ashton Rangers sare ya bao 1-1 katika uwanja wa ugenini kwenye derby la Changamwe.

Beach Bay pia nao walizimishwa sare ya bao 1-1 na Shimanzi fc, Wakati vijana wa Juma Kalato Omax FC wakipiga sare ya 1-1 dhidi ya vijana wa watamu Inter Dabaso.

Na hatimaye Deep Sea kutoka Lamu inayoongozwa na mkufunzi Athman Pirezi ilitandikwa nyumbani kwao na Ziwani Youth kichapo cha mabao 3-2 katika uwanja wa Lamu Sports Ground.