TUKO TAYARI KUIWAKILISHA KENYA KIMATAIFA – OLUNGA

Nahodha wa timu ya taifa ya Harambee stars Michael Olunga ameeleza kufurahishwa kwake na shirikisho la soka nchini kwa maandalizi ya mechi ya kirafiki dhidi ya Iran katika jaribio la kujipima uwezo wao katika ushuindani wa kimataifa.

Harambe stars ambao mara ya mwisho kucheza mechi ya kimataifa ilikuwa mwaka 2021 dhidi ya Rwanda wamekuwa nje kutokana na kufungiwa kimataifa na shirikisho la soka baada ya serikali kuingilia masuala ya shirikisho la soka.

Kenya, Harambe Stars watakuwa wanashuka dimbani kesho dhidi ya Timu ya taifa ya Iran na Olunga anasema kwa hatua hiyo ni nafasi muruwa ya kuonyesha uwezo wao baada ya kipindi kirefu bila jukumu la kitaifa.

Kwa upande wake mkufunzi mkuu wa kikosi hicho Engin Firat ametetea uamuzi wa kumuacha nje Benson Omala wa klabu ya Gor Mahia akisema kwamba bado kuna nafasi kubwa kwa vijana wacha kuimarika katika kikosi chake katika katika siku za usoni.