TUNACHEZA KUJIPIMA – ENGIN FIRAT

Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Harambee stars anasema kuwa mechi ya kirafiki dhidi ya Iran itakayochezwa usiku wa leo ni ya kujipima nguvu na uwezo wao katika mashindano ya kimataifa.

Harambe Stars tayari wako Iran na watakuwa wanashuka dimbani na Iran ambao wanasimama katika nafasi ya 21 katika viwango vya fifa na mkufunzi Firat anasema kwamba mpinzani huyo ni sahihi kabisa kutambua wanasimama wapi kimataifa watakapo jipima usiku wa leo.

Kenya ama Harambe stars leo wanacheza mechi ya kwanza kimataifa tangu mwaka 2021 kutokana na kufungiwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na fifa baada ya serikali ama wizara ya michezo iliyokuwa inayongozwa na aliyekuwa waziri Amina Mohamed kuingilia masuala ya shirikisho la soka nchini Kenya.