U-TURN KUANDAA MASHINDANO YA ‘SOKA LA YESU’ TENA

Kikundi cha wainjilisti cha U-Turn Society mjini Malindi kaunti ya Kilifi kwa ushirikiano na kanisa la Life Church International Malindi kinalenga kuandaa mashindano ya soka yanayojulikana kama Mbuzi Football Tournament mwezi huu.

Kulingana na waandalizi wa mashindano hayo ni kwamba lengo kuu ni kukuza vipaji vya vijana pamoja na kueneza injili ya Yesu Kristo kwa vijana wa mji wa Malindi kaunti ya Kilifi.

Ni mashindano ya siku moja ya vijana wachanga ambayo yatafanyika tarehe 17 mwezi huu katika shule ya Msingi ya Central mjini Malindi.

Mashindano hayo yanakuja baada ya mashindano ya mwaka jana ya ‘Soccer for Jesus’ yaliyofanyika mwaka jana katika ufukwe wa Bunthwani katika mji wa Malindi. Timu kadhaa ikiwemo kikosi cha wanahabari wa Lulu fm walishiriki na timu yao ya wachezaji saba kila upande.

Katika mashindano hayo kulikuwepo na wahubiri ambao walitangaza injili ya Yesu kwa vijana walioshiriki kutoka matabaka tofauti katika jamii ya mji huo.