Klabu ya Tottenham Hotspurs sasa ni rasmi imempa kazi ya ukocha mkufunzi Ange Postecoglou kwa kumpa mkataba wa miaka minne kuiongoza klabu hiyo ya London.
Postecoglou mwenye umri wa miaka 57 anachukua mikoba ya Spurs baada ya kuwa na kiwango bora na Celtic ambako ameshinda mataji matatu ya ndani ya ligi kuu ya Scotland msimu huu.
Anavaa viatu vya mkufunzi Antonio Conte aliyejiuzulu mwezi Machi kwa makubaliano ya pande zote mbili. Taarifa za awali zilikuwa zasema kwamba mkufunzi Conte aliondoka klabuni hapo kutokana na kukosa heshima miongoni mwa wachezaji pamoja na kuwa na mgawanyiko katika klabu hiyo.
Alikiri katika moja ya mahojiano na vyombo vya habari kwamba wachezaji wa Spurs akiwaongoza walikuwa wavivu mno pamoja na baadhi kukataa kurekebishwa wanapokosea uwanjani.

