HARAMBEE STARS WANOGESHA MAZOEZI

Timu ya taifa ya Harambe Stars imeingia katika siku yake ya pili katika kambi ya mazoezi kwa matayarisho ya mashindano ya mataifa manne yatakayofanyika nchini Mauritius.

Mashindano hayo yataanza rasmi siku ya jumapili ijayo tarehe 11 mpaka 18 na yanahusisha Kenya, Djibouti, Mauritius pamoja na Pakistan.

Timu ya Harambe stars inalenga kusafiri kuelekea Maurituois wikendi ijayo kwa ajili ya mashindano hayo.

Mashindano mengine ya Harambe Stars kushiriki mwaka huu ni mashindano ya kutafuta tikiti ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2026 nchini Benin.