KUFIKA FAINALI NI TUKIO KUBWA MAISHANI MWANGU, TUTAMALIZA UKAME WA MAKOMBE – DAVID MOYES

Mkufunzi wa klabu ya Westham United David Moyes anasema kufika fainali ya Europa Conference league ni tukio kubwa kutokea katika kazi yake ya ukufunzi.

Ameyasema hayo kipindi ambacho Westham usiku wa leo watakuwa wanashuka dimbani dhidi ya Fiorentina katika fainali ya Europa Conference league.

Amesema Westham United usiku wa leo wanalenga kushinda ubingwa wao wa kwanza baada ya miaka 43.

Mara ya mwisho kwa wananyundo hao kushinda ubingwa wowote ilikuwa mwaka 1976 na walishinda ubingwa wa kombe la FA dhidi ya klabu ya Manchester United.