Waandalizi wa mashindano ya soka ya Mbuzi Football Tournament (U-Turn na Life Church International Malindi) yanayolengwa kufanyika wiki ijayo katika shule ya msingi ya Central mjini Malindi kaunti ya kilifi wanasema kwamba mashindano hayo yanazidi kuvutia vilabu vingi mashinani.
Mashindano hayo yanayolenga kueneza injili ya Yesu Kristo kwa vijana wa eneo la Malindi yalifaa kuhusisha timu sita lakini sasa maombi ya vilabu kuomba kushiriki yanazidi kuongezeka.
Ni Mashindano ambayo mshindi atakuwa anajishindia mbuzi sawia tu na nafasi ya pili pamoja na timu zote kupata nafasi ya kipekee ya kuhubiriwa injili ya Yesu Kristo.
Kulingana na mwanzilishi wa kikundi wa wainjilisti cha U-turn Andrew Obara ni kwamba usajili wa vilabu vinavyotaka kushiriki mashindano hayo kwa sasa upo wazi ili kuona kwamba vilabu vingi zaidi vinahusika katika mashindano hayo ya soka.
”Kwa sasa tumekuwa tukipokea simu nyingi za maombi hasa upande wa Pastor Danny Gift watu wanasema tuongeze timu ziwe nyingi. Mpango wetu ulikuwa tuhusishe timu sita pekee za wachezaji nane kila upande lakini sasa maombi yanazidi kuongereza” Alisema Anthony Obara.
” Kukijaa watu zaidi ndio vizuri kwetu kwa sababu tutamtangaza Yesu kwa watu wengi zaidi. Kwa hivyo sisi tunataka watu wazidi kujisajili ili wakati huo Yesu apate umati vizuri. Hii Malindi lazima tuhubiri injili mpaka kukae sawa.” Aliongeza Anthony.

