Mkufunzi wa muda wa klabu ya Bandari FC Twahir Muhiddin ameeleza kuridhika kwake na mabadiliko ya kikosi alichonacho kwa sasa katika ligi kuu ya FkF.
Wikendi ilopita Bandari ya Muhiddin ilishinda iliishinda Sofapaka kwa kichapo cha mabao 2-0 katika uwanja wa Nyayo.
Kufikia sasa chini ya Uongozi wa Muhiddin Bandari imecheza mechi 6 bila kupoteza, wameshinda mara nne na kupiga sare mara mbili.
Bandari kwenye ligi inasimama katika nafasi ya 6 wakiwa na alama 54. Mechi zao za mwisho ni dhidi ya Kariobangi Sharks na Posta Rangers.
Msikilizaji, katika ligi kuu ya Kenya msimu huu mshindi atakuwa anaenda nyumbani na kikombe tu bila pesa baada ya fkf kutangaza kuwa hawana pesa za kutuza mabingwa.

