Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid analenga kuyoyomea Saudi Arabia katika uhamisho ujao baaba ya kuchezea Real Madrid tangu mwaka 2009 aliposajiliwa kuka Lyon ya Ufaransa.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ameshinda mataji 25 akiwa Santiago Bernabou na sasa ripoti za soka ulaya zadai kwamba anakaribia kupewa ofa nono kutoka klabu ya Al Ittihad.
Mwengine ambaye atakuwa anayoyomea klabu ya milki za kiarabu ni Lionel Messi ambaye ni mshindi wa kombe la dunia. Kulingana na ripoti kutoka Paris Ufaransa zasema kwamba Messi hatakuwa mchezaji wa PSG msimu ujao.
Maafisa wa klabu ya Al Hilal wanaripotiwa kusafiri hadi Ufaransa kujaribu kukamilisha dili hilo na Messi amepewa ofa nono ili kukamilisha uhamisho huo.
Nahodha wa klabu ya Manchester City Ilkay Gundogan yuko mbioni kujiunga na Barcelona mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto, huku klabu hiyo ya La Liga ikimshawishi kiungo huyo wa kati wa Ujerumani, 32, kwa ofa ya mkataba wa miaka mitatu.
Mshambuliaji huyo aliandikisha historia wikendi hii kwa kufunga bao la haraka zaidi katika mashindano ya kombe la FA kwa kufunga bao la kwanza katika sekunde ya 12 kwnye fainali ambayo Manchester City waliishinda Manchester United kwa mabao 2-1 na kushinda ubingwa wa FA.

