Tuzo za mchezaji bora wa soka zinatarajiwa kufanyika usiku wa leo (Jumatatu) katika ukumbi wa Palais des Congrès in Marrakech, Morocco na kwa wakati mwengine zimevutia washindani wakali.
Victor Osemhen mchezaji raia wa Nigeria pamoja na klabu ya Napoli kule Italia ambaye msimu jana aliisaidia klabu yake kushinda ubingwa wa taji hilo baada ya miaka mingi anashindanishwa na Mohamed Salah winga wa Mirsi pamoja na klabu ya Liverpool kule Uingereza.
Mwengine ambaye anangangania tuzo hilo ni AcHRAF Hakimi aliyeisaidia Morocco kumaliza katika nafasi ya nne kwenye kombe la dunia pamoja na kushibnda kombe la France League One kule Ufaransa na klabu yake ya sasa Paris Saint Germain.
Kwa kweli ni tuzo zenye ushindani lakini tusubiri mbivu na mbichi na tutakuwa tunakujuza kumekwendaje huko

