Tuzo za Caf za wachezaji bora wa kiume na kike zilifanyika wiki hii (Jumatatu) katika taifa la Morocco. Victor Osemhen mchezaji wa klabu ya Napoli kule Italia na taifa la Nigeria ndiye mchezaji bora wa soka wa kiume huku Asisat Oshoala ambaye ni mchezaji mwenzake wa Nigeria akishinda tuzo la mchezaji bora wa kinadada mwaka huu.
Timu bora ya mwaka barani Afrika ni Morocco baada ya kuandikisha matokeo mazuri katika mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika nchini Qatar ambako walimaliza katika nafasi ya nne mwaka jana.
Tuzo hizo zimemshuhudia Yassine Bounou kipa wa zamani wa Sevilla na timu ya taifa ya Moorocco akishinda tuzo la kipa bora wa mwaka.
a ndiye mchezaji bora wa soka wa kiume huku Asisat Oshoala ambaye ni mchezaji mwenzake wa Nigeria akishinda tuzo la mchezaji bora wa kinadada mwaka huu.
Wengine waliopata tuzo ni;
Walid Regragui (Morocco) – mkufunzi bora wa mwaka
Lamine Camara – mchezaji bora mchanga wa kiume
Al Ahly – klabu bora ya kiume
Mamelodi Sundowns Ladies FC – Klabu bora ya kinadada
Desiree Ellis – Kocha bora wa kike
Timu ya taifa ya Nigeria (Kinadada) – Timu bora ya taifa

