TUTAWAKILISHA TANA RIVER VYEMA, MKUFUNZI JILLO AAHIDI

Mkufunzi mkuu wa kikosi cha Sango Sportiff klabu pekee inayowakilisha kaunti ya tana river katika ligi ya daraja la pili kitaifa  amekiri kwamba matayarisho duni ndio chanzo cha kuwa na mwamnzo mbaya msimu huu.

Mkufunzi Righo Jillo wakati akizungumza na tama la spoti uwanjani Alaskan baada ya kupiga sare tasa dhidi ya klabu ya Yanga wikendi iliyopita amethibitisha kuwa vijana wake walikumbwa na changamoto nyingi mwanzoni mwa msimu jambo ambalo lililemaza juhudi zao za kuonyesha kiwango kizuri katika ligi.

Sango Sportif  hadi kufikia sasa wamesajili ushindi mmoja pekee katika mechi sita za kwanza katika ligi hiyo na Jillo ameeleza matumaini kwamba kikosi chake kitaimarika na kuanza kutoa matokeo mazuri katika mechi zijazo.