Mkufunzi Nero Chishenga wa klabu ya Furunzi FC anaeleza kutoridhika na matokeo ya vijana wake katika mechi ya ugenini wikendi hii dhidi ya klabu ya Shimanzi FC mjini Mombasa ambapo Furunzi walitandikwa kichapo cha mabao 5-1.
Nero amedokezea Tama la Spoti kwamba kulishuhudiwa maonevu kutokana na waamuzi wa mechi hiyo hali ambayo anahoji kuwa kinyume kabisa na ustaarabu wa soka.
Katika mechi hiyo Furunzi walipigwa kadi saba za njano katika hali isiyobainika akisema kwamba jambo hilo lilikatisha tama wachezaji wake.
Kwa sasa Furunzi fc katika ligi ya daraja la pili kitaifa inasimama katika nafasi ya 6 wakiwa na alama nane baada ya mechi 6.

