Doris Petra ambaye ni naibu rais wa shirikisho la soka nchini kenya amethibitisha bayana kwamba Charles Okeree ataendelea kuwa mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya kina dada ya Harambe Starlets.
Hii ni kufuatia kuibuka kwa sintofahamu baada ya kamati ya mpito iliyokuwa chini ya waziri amina Mohamed kumfuta Okere na kumtwika majukumu Alex Alumira kuongoza wanadada hao.
Baada ya Serikali mpya na wizara mpya ya Ababu Namwamba kuingia, lakini pia marufuku ya fifa kuondolewa Okere ambaye ni naibu mkufunzi wa zamani wa klabu ya Tusker atarejea kwenye majukumu yake. Yote haya yanafanyika baada ya shirikisho la soka kuharamisha kazi zote zilizofanywa kipindi cha kamati ya mpito iliyobuniwa na waziri Amina.

