CHRISTIAN ATSU ANUSURIKA UTURUKI

Naibu Rais wa klabu ya Hatayspor Mustafa Ozat amethibitisha kwamba Christian Atsu mchezaji wa klabu hiyo amenusuriwa akiwa na majeraha kutoka kwenye vifusi vilivyosababishwa na mtetemeko wa ardhi uliotokea kusini mwa taifa ya Uturuki.

Hata hivyo mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Taner Savut anasalia kukwama katika vifusi huku juhudi za kuokoa watu zikiendelea.

Kufikia sasa kulingana na taarifa za baadhi ya vituo vya habari ulaya ni kuwa watu zaidi ya 5000 wamepoteza maisha yao pamoja na nyumba takriban elfu sita zikibomoka, mali kuharibika yote kutokana na mtetemeko wa ardhi uliotokea jana.