Mkufunzi mkuu wa klabu ya Gor Mahia JohnNathan McKinstry anasema kwamba anaimani kuwa ya kutetea ubingwa wa kombe la Mozzert Bet ambalo awali lilijulikana kama FKF Cup kabla ya kupatikana kwa mdhamini.
Mkufunzi huyo anasema kwamba kama klabu wamefanya mabadiliko ya kutosha katika kikosi hicho jambo ambalo liliwafanya kusajili ushindi wa bao 1-0 wikendi ilopita dhidi ya Kibera soccer, ushindi ambao sasa umewasongesha hadi hatua ya 16 bora ya mashindano hayo na wameratibiwa kuvaana na Kakamega Homeboyz.
Vijana wa Kakamega walifuzu kuingia 16 bora kupitia mikwaju ya penalty kwa kuitandika klabu ya Shalimar mabao 4-3.

