Vilabu vya mashinani vimeonywa kutosajili wachezaji wa ligi nyingine bila taarifa rasmi za usajili kupitia shirikisho la soka la fkf.
Katika taarifa iliyochapishwa mitandanoni na katibu wa soka la Malindi kaunti ya Kilifi bwana Lucas Bahati ni kwamba vilabu vitakavyokiuka sheria za uhamisho vitachukuliwa hatua vilivyo.
Haya yanajiri kipindi ambacho baadhi ya vilabu vya soka mashinani katika eneo bunge hilo vimeanza kusajili wachezaji kutoka vilabu vya ngazi za juu ili kusaidia vilabu hivyo kuandikisha matokeo mazuri kwenye msimu mpya wa mwaka 2022/2023 ulioanza rasmi wikendi ilopita.

