FIKIRINI JACOBS AMKOSOA WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA MOSES KURIA

Kiongozi wa vijana katika kaunti ya Kilifi Fikirini Jacobs amemtaka waziri wa biasahara na viwanda nchini Moses Kuria kujitenga na masuala yanayohusiana na wizara ya elimu.
Fikirini anadai Kuria amechochea kubinafsishwa kwa vyuo vikuu nchini hali ambayo anasema itaathiri vyuo vya umma katika taifa hili la Kenya.
Amesema iwapo wizara ya elimu itaanza kuingiliwa huenda sekta hiyo ikadorora hata zaidi.