TUTALETA VIFAA VYA MICHEZO MASHINANI – JACINTA MBEYU

Rais wa bunge la vijana katika kaunti ya Kilifi Jacinta Mbeyu ametoa hakikisho kwamba bunge la kaunti hiyo linalenga kutengeneza klabu ya mpira ya kaunti ambayo itawakilisha kaunti nzima katika mashindano mbalimbali ya soka.

Kulingana na Mbeyu ni kuwa wizara ya michezo pamoja na mkurugenzi mkuu wa michezo katika kaunti hii wameanza mchakato wakuwinda talanta za vijana ambao watajumuishwa kutengeneza kikosi imara cha kaunti.

Jacinta amesema kwamba bunge hilo pia linaendelea na mchakato wa kupitisha miswadaya kushinikiza serikali kutenga bajeti ya kupeleka vifaa vya michezo mashinani ili kusaidia wachezaji kukuza talanta zao viwanjani.