Mechi ya kutafuta msindi wa tatu na wanne katika mashindano ya mataifa bingwa Afrika maarufu kama CHAN itakuwa inarindimwa usiku wa wa leo ambapo timu ya taifa ya Madagascar itakuwa inashuka dimbani dhidi ya Niger saa nne usiku.
Fainali za mashindano hayo zitakuwa zinachezwa kesho ambapo timu ya taifa ya Algeria, waandaaji wa mashindano haya watakuwa wanashuka dimbani dhidi ya mabingwa wa AFCON 2020 waite Senegal maarufu kama simba wa teranga.
Ikumbukwe kwamba timu ya taifa ya Morocco ambao waliweka historia katika mashindano ya dunia mwaka jana walikosa kushiriki katika mashindano ya CHAN kutetea ubingwa wao mwaka huu kutokana na kukosa kuridhiana na wenyeji Algeria katika masuala mazima ya usafiri wa ndege.

