KLABU YA VIHIGA BULLETS MASAIBU TELE LICHA YA KUDHAMINIWA NA KAUNTI

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Vihiga Bullets George Owoko ametoa wito kwa wahisani kusaidia klabu hiyo ya ligi kuu nchini Kenya kipindi hiki ambacho klabu hiyo inapitia kipindi kigumu kifedha.

Ukosefu wa udhamini bado unasalia kuwa saratani katika soka la Kenya na mkufunzi huyo ameomba shirikisho la soka pia kuwapiga shime ili kushiriki mechi zote za ligi bila kukosa kuheshimu ratiba jambo ambalo huenda likawaweka pabaya.

Ikumbukwe kwamba klabu ya Vihiga Bullets iliundwa na aliyekuwa gavana wa vihiga Moses Akaranga na baadaye kuchukuliwa rasmi na serikali ya kaunti wakati wa gavana wa sasa Wilberforce Otichillo lakini hadi sasa klabu hiyo haijapokea hela au usaidizi wowote wa usafiri.