TUSKER YAJITAYARISHA KWA MSIMU MPYA

Mkufunzi wa wanamvinyo Tusker FC mwite Robert Matano amesema kwamba kambi yake iko imara wanapojitayarisha kwa msimu mpya na wachezaji wapya waliowasajili katika dirisha la uhamisho lililofungwa wiki jana.

Kulingana na Matano uongozi wa klabu hiyo umewasaidia kuunda kikosi kitakachowawezesha kungangania taji la ligi kuu msimu ujao ambao huenda ukawa ubingwa wao wa tatu mfululizo katika historia.

Ligi ilifaa kuanza tarehe 24 mwezi huu kulingana na kamati ya mpito inayosimamia soka nchini huku Rais Nick Mwendwa ambaye alitangaza rasmi wiki jana kwamba amerejea kwenye ofisi yake alidokeza kupitia mtandao wake wa twitter kwamba ligi itaanza mwezi ujao.

Kwa sasa Tusker inajitayarisha kwa mechi mbili za kirafiki kati yao na Gusii United inayochezea ligi ya National Super League na baadae kukipiga dhidi ya APS Bomet.