Mkufunzi mpya wa klabu ya Chelsea Graham Potter anatarajiwa kuanza jukumu lake la kwanza na klabu yake mpya darajani Stamford Bridge jioni ya leo wakati ambapo the Blues watakuwa wanavaana na RB Salzberg katika mechi ya pili ya hatua ya makundi.
Chelsea ilimfuta kazi mkufunzi wao Tomas Tuchel baada ya kichapo cha aibu cha bao 1-0 dhidi ya Dynamo Zagreb ya taifa la Croatia na sasa kibarua kizito kinatarajiwa kwa Graham Potter kuwasaidia mabingwa hao waliowahi kutwaa taji la klabu bingwa ulaya mara mbili kuingia katika hatua ya mchujo.
Graham Potter anaachana na Brighton inayoshiriki ligi kuu nchini uingereza katika nafasi ya nne na alama 12 na rekodi ya kihistoria kwenye klabu hiyo ya kumaliza katika nafasi ya tisa msimu uliopita na ni mkufunzi mwenye uzoefu wa ligi kuu nchini uingereza baada ya kukiongoza kikosi cha brighton kwa misimu miwili mfululizo.

