Rais William Ruto anatarajiwa kuwaapisha majaji wanne miongoni mwa majaji sita walioteuliwa miaka mitatu iliyopita baada ya kuwaidhinisha hapo jana.
Kwenye hotuba yake ya kwanza kufuatia kuapishwa kwake kuwa rais wa taifa hili, Rais Ruto alihoji kuwa hafla hiyo ya kuapisha majaji hao itafanyika katika ikulu ya Nairobi.
Majaji hao ni pamoja na Aggrey Muchelule, George Odunga, Weldon Korir, prof. Joel Ngugi waliokuwa mahakama kuu waliteuliwa kujiunga na mahakama ya rufaa huku tume ya JSC ikipendekeza majaji evans Makori na Judith Omange kupandishwa vyeo na kujiunga na mahakama ya mazingira na ardhi.
MAJAJI SITA WALIOTEULIWA MIAKA MITATU ILIYOPITA KUAPISHWA

