TUKO NA IMANI NA GAVANA WA SASA KATIKA MICHEZO – MWABATI

Mwenyekiti wa klabu ya Young Bulls Jonson Mwambati amesema kwamba ako na matumaini makubwa na serikali ya kaunti ya kilifi katika kuimarisha michezo mashinani katika siku za usoni.

Mwambati amesema kwamba kama wanamichezo katika kaunti ya kilfi wana matumaini makubwa na gavana wa sasa Gedion Maitha Mungaro kwamba atasaidia ukuaji wa talanta na michezo kupitia ujenzi wa miundo msingi kama vile viwanja.

”Tuko na matumaini makubwa na gavana wa sasa. Ukiona serikali yake inashuka mpaka mashinani kuja tazama mechi kama hivi (kwenye Mudzini dabi) basi inaonyesha ishara nzuri kwamba mambo yatakuwa mazuri. Huu ni mwaka wake wa kwanza wa kifedha na tunajua atapanga mambo ikiwemo ujenzi wa viwanja ili vijana wetu wazidi kuboresha talanta zao.” Alisema Mwabati.

Katika dabi ya wikendi iliyopita Young Bulls walishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Malindi Progressive na kuwafanya kuzidi kuselelea katika uongozi wa ligi ya daraja la kwanza kitaifa.

Mechi hiyo licha ya kwamba ilichezwa katika kipindi cha mvua katika dakika zote tisini mashabiki walijaa uwanjani kutazama mechi hiyo kubwa katika uwanja wa Malindi Alaskan.