Mmiliki mpya wa klabu ya Chelsea, Todd Boehly amesema kwamba uamuzi wa kumfuta kazi mkufunzi Thomas Tuchel hauhusiani kabisa na kupoteza kwa mechi ya klabu bingwa dhidi ya Dynamo Zagreb wiki iliyopita.
Bilionea huyo wa Marekani amesema kwamba kama klabu walikuwa na malengo ya kuanza safari mpya ya kukarabati kikosi hicho kuanzia juu mpaka wachezaji wa akademia na kufanya marekebisho ya kumleta mkufunzi Graham Potter ilikuwa mbinu moja wapo ya kuleta sura mpya ya klabu hiyo ya darajani.
Pamoja na marekebisho hayo ameongeza kuwa Chelsea kama biashara yake lengo kubwa lake ni kufanya mabadiliko ambayo yataendana na mfumo pamoja na filosofia zake kuhusu ufanisi wa klabu hiyo.
Kwa upande wake mkufunzimpyawa Chelsea Graham Potter baada ya mechi yake ya kwanza alisema kuwa kama klabu bado wako na safari ndefu ya kufanya marekebisho kwenye kikosi hicho katika idara tofauti tofauti ili kungangania mataji msimu huu.
Katika mechi ya klabu bingwa ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo Chelsea imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya RB Salzburg katika uga wao wa Stamford Brigde.

