BERNARD MWALALA ASAJILIWA NA ULINZI STARS

Klabu ya Ulinzi Stars imemsajili Bernard Mwalala kama mkufunzi wao mpya klabu hiyo inapoelekea msimu mpya wa mwaka 2022/2023.

Mwalala ambaye sasa anachukua nafasi ya Benjamin Nyangweso katika uongozi wa klabu hiyo atasaidia na Vincent Otieno pamoja na mkufunzi Hamisi Abdalla.

Mkufunzi Mwalala sasa atachukuwa majukumu ya kukiongoza kikosi hicho katika mechi za kirafiki kabla ya mwanzo wa msimu mpya ambao unatarajiwa kuanza tarehe 24 mwezi huu.

Ulinzi stars waliomaliza katika nafasi ya 13 msimu uliopita, wataanza msimu mpya watakapokuwa wanashuka dimbani dhidi ya APS ambao walipanda daraja msimu huu kutoka national super league.

Bernard Mwalala msimu uliopita aliisaidia klabu yake kakamega homeboyz kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya wanamvinyo tusker fc kwa utofauti wa mabao kabla ya kufutwa na uongozi wa klabu hiyo.