PAUL BITOK ANAIMANI MALKIA STRIKERS WATAFANYA VYEMA KWENYE MASHINDANO YA DUNIA

Mkufunzi mkuu wa Malkia Strikers Paul Bitok anaimani kwamba wanadada hao watafanya vyema katika mashindano ya dunia ya mpira wa wavu yanayotarajiwa kufanyika tarehe 23 mwezi huu hadi 15 mwezi October katika taifa la Uholanzi pamoja na Poland.

Bitok amesema kwamba mazoezi ya miezi miwili waliyopiga kambi katika taifa la Brazil yamewasaidia kuimarika zaidi na sasa kikosi hicho kinatarajiwa kusafiri kuelekea Uholanzi tarehe 20 mwezi huu kabla kucheza mechi yao ya kwanza dhidi ya taifa hilo la Uholanzi katika mechi yao ya kwanza tarehe 23.

Katika mashindano hayo Malkia Strikers pia wameratibiwa kuvaana na mabingwa wa Afrika taifa la Cameroon tarehe 27 kabla ya kuvaana na Italia katika mechi za kwanza za mashindano hayo.