KALONZO MUSYOKA ATOA WITO KWA RAIS RUTO KUIPA IDARA YA MAHAKAMA FEDHA ZA KUTOSHA

Kinara wa chama cha WIPER Kalonzo Musyoka ametoa wito kwa Rais William Samoei Kipchirchir Arap Ruto kuipa idara ya mahakama fedha za kutosha ili kutekeleza majukumu yake bila changamoto zozote.
Katika taarifa yake kwa wenyeji wa kaunti ya Mombasa kwenye hafla ya kuapishwa kwa gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir, amesema taifa la Kenya linahitaji idara ya mahakama ambayo ni huru na ambayo haidhibitiwi na rais wa Nchi.
Vilevile, amempongeza Rais Ruto kwa kutia saini amri ambayo inaipa idara ya Polisi uhuru wa Kifedha na kutaka hilo pia kufanyika kwenye idara ya mahakama.