Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Abdalla Timamy amesema zaidi ya wafanyikazi hewa 200 kwenye serikali ya kaunti hiyo wamesimamishwa kazi.
Amesema hatua hiyo inapania kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa serikali ya kaunti hiyo zinatumika katika masuala ambayo yatawanufaisha wenyeji ikiwemo miradi ya maendeleo.
Kwa mujibu wa Gavana huyo a maafisa wa idara mbalimbali kwenye serikali ya kaunti hiyo watapunguzwa hadi 11.
ZAIDI YA WAFANYIKAZI HEWA 200 WASIMAMISHWA KAZI KAUNTI YA LAMU

