BAA LA NJAA LAZIDI KUWAATHIRI WENYEJI WA MRIMA WA NDEGE KAUNTI YA KILIFI

Chifu wa eneo la Mrima wa Ndege wadi ya Sokoke kaunti ya Kilifi Samson Karisa anasema kuna haja ya msaada wa dharura wa chakula cha msaada kupelekewa wakazi wa sehemu hiyo.
Kulingana na Karisa  wakazi wa sehemu hiyo wanaendelea kuteseka kutokana na njaa, kwasababu ya ukosefu wa chakula baada ya mvua kukosa kunyesha .
Karisa anasema ni takribani miezi minne kufikia sasa hawajapata msaada  wowote wa chukula cha msaada kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kilifi.
Wakati huohuo ameitaka serikali kuhakikisha inaweka mikakati ya kupunguza bei ya bidhaa muhimu nchini.