Idadi kubwa ya kesi dhidi ya mauaji ya wazee katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi, zinadaiwa kukosa kuendelezwa mahakamani, kutokana na ukosefu wa ushahidi wa wale wanaotekeleza visa hivyo.
Ni kuali ya viongozi wa jamii ya kimijikenda katika muungano wa kitamaduni Malindi District Cultural Association (MADCA), ambao wamesema licha ya baadhi ya wanajamii kufika mahakamani kama mashahidi wa kesi hizo, wengi wao wamekosa kuwataja wale wanaotekeleza visa hivyo.
Wakizungumza na wanahabari katika zoezi la kuangazia kesi hizo kwenye kituo cha hifadhi ya wazee hao eneo la Moi eneo bunge la Magarini, viongozi hao wakiongozwa na katibu wao Joseph Mwarandu, Stanely Kiraga pamoja na Edward Kazungu, wasema kuwa hatua hiyo imechangiwa na wanajamii kuhofia maisha yao, baada ya wao kuweka wazi majina ya vijana wanaohusiaka, katika mauaji ya wazee kwa tuhuma za uchawi kwenye jamii.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa kituo cha kutetea haki za kibinadamu MALINDI HUMAN RIGHTS, Victor Kaudo amesema kuwa kituo hicho sasa kitaanza kuangaziA kesi hizo kwa ushirikiano na afisI ya mkurungezi mkuu wa mashta ya uma ODPP katika eneo la Malindi, ili kuhakikisha kuwa wazee walionusurika kifo katika kituo hicho wanapata haki.
UKOSEFU WA USHAHIDI WACHANGIA KWA KESI DHIDI YA MAUAJI WA WAZEE ENEO LA MALINDI KUCHUKUA MUDA ZAIDI

