Takribani watu 12 tayari wamewasilisha maombi yao ya kuwania wadhifa wa Uspika katika bunge la kaunti ya Kilifi.
Kulingana na bunge hilo baadhi ya wale ambao wako kwenye kipute hicho ni aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Garashi Peter Ziro, Aliyekuwa mbunge wa Ganze Teddy Mwambire, James Charo Mulewa, Stanley Saburi, Carolyne A. Chilango, Paul Chivatsi Chai, Larry Chiringa Mbega, Emmanuel Kiseleve Nzivo na Gilbert Peru.
Kwenye kipute cha kuwania wadhifa wa naibu spika ni jumla ya watu watano ambao wamejitokeza ambao ni Twaher Abdulkarim, Martha Koki, Nafthali Kombo, Thaura Mweni na Agnes Sidi.
Watakaofaulu watapigiwa kura kesho Jumanne katika bunge la kaunti ya Kilifi baada ya wawakilishi wa wadi kuapishwa rasmi.
TEDDY MWAMBIRI NI MIONGONI MWA WANOWANIA WADHIFA WA USPIKA WA BUNGE LA KILIFI

