MAANDAMANO YA AMANI KUANDALIWA HADI KWENYE BANDARI YA MOMBASA

Mwenyekiti wa vuguvugu la First Action kaunti ya Mombasa Salim Karama amesema siku ya Jumatano wiki hii wataandaa maandamano ya amani hadi katika bandari ya Mombasa kufuatia agizo la rais William Samoei Kipchirchir Arap Ruto la kuregesha huduma za bandari kwenye bandari hiyo kutoka ile ya Naivasha.
Karama amewataka wenyeji pamoja na wafanyabiashara kujitongeza kwa wingi siku ya Jumatano kwa maandamano hayo ya amani kama ishara ya shukrani kwa Ruto kwa kutimiza ahadi yake ya kutekeleza hilo wakati wa kampeni zake za kisiasa.
Amesema hatua hiyo ya kuregeshwa kwa huduma hizo kutachangia kubuni nafasi za kazi kwa vijana kwenye kaunti hiyo na kanda ya pwani kwa jumla.