Afisa ambaye anasimamia hifadhi ya WATAMU MARINE PARK kaunti ya Kilifi Dadley Tsiganyiu amewahimiza wenyeji kulinda mazingira ya baharini kwa kusitisha utupaji ovyo wa taka kwenye fuo za bahari hindi.
Akizungumza katika eneo hilo amewataka kuokota taka za plastiki zilizoko kwenye fuo za bahari na kisha kuzipeleka katika kituo cha ECO – WORLD ili zinunuliwe wapate fedha.
Amesema utupaji wa plastiki ndani ya bahari, unaathiri maisha ya viumbe wa baharini.
Naye Zena Mohamed ambaye ni mkurugenzi wa masuala ya mazingira kaunti ya Kilifi amesema mikakati imewekwa ili kuhakikisha wenyeji wananufaika na taka za plastiki.
WENYEJI WA WATAMU WATAKIWA KUOKOTA TAKA ZA PLASTIKI KWENYE FUO ZA BAHARI

