Kiungo wa Harambee Stars Timothy Babu Ouma amekamilisha uhamisho wa kipekee kuelekea klabu ya jamhuri ya Czech Slavia Prague, hii ni baada ya Kuachana na upande wa Uswizi IF Elfsborg, kwa dili ya aina yake ya takriban milioni mia nne sabini na tatu pesa Taslim Ya Kenya.
Mzawa Huyo Wa kariobangi ambaye amewahi kukipiga na Nairobi City Stars amekua Kiungo kikuu cha Elfsborg msimu huu, akijipakulia nafasi yake kwenye Kikosi Cha kwanza, huku akifanya Vyema kwenye michuano ya Europa.
Babu Tayari Amekamilisha vipimo vya Afya na Slavia Prague, ambao wameratibiwa kumenyana na Malmo FF siku ya Alhamisi kwenye michuano ya Europa, nao Elfsborg wakizichapa na Tottenham Hotspurs.

