Mwenyekiti wa timu ya Kisimu Ndogo United Ali Best anasema ipo haja ya serikali ya kaunti za kaunti ya Kilifi na ile ya Kwale kuingilia kati na kuzinasua klabu za Young BULLS na SS Assad kipindi hiki kigumu kwao kiuchumi.
Best ameyasemahayo baada ya wiki jana klabu ya SS Assad kutangaza na kufeli pia kushiriki mechi yao ya ugenini dhidi ya MOFA kwa kushindwa kugharamia safari hiyo.
Best amesistiza haja ya serikali kutenga fedha za kutosha michezoni ili kusaidia malezi ya soka za vijana iwapo wangependa kuona soka likisonga mbele.
Best ambaye klabu yake ya Kisumu ndogo United inazidi kujiandaa kwa msimu mpya wa ligi ya mkoa baada ya kushindwa kupanda daraja msimu jana ametoa wito kwa viongozi mbalimbali hasa gavana wa kilifi kuingilia kati masaibu ya Young Bulls ambayo imedorora kiviwango msimu huu kutokana na ukata wa kifedha.

