Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, amewaonya viongozi wa bara Afrika dhidi ya kulalamimikia uamuzi wa Rais wa Marekani, Donald Trump kubadili sheria nchini humo, ambazo zitakuwa na athari kwa mataifa ya bara Afrika.
Kwa mujibu wa Uhuru, licha ya mataifa ya Afrika kuwa na rasilimali nyingi zilizo na uwezo wa kufadhili mataifa hayo kiuchumi, masuala ya ufisadi yamekuwa yakichangia pakubwa ukosefu wa fedha katika mataifa hayo.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa kwenye kongamano la afya, linalo husisha mataifa ya Afrika Mashariki, Kenyatta amesema kuwa mataifa hayo sasa yanapaswa kufanya mzungumzo, ya jinsi gani yanaweza jisimamia katika utendakazi wake.
Kenyatta amesisitiza kuwa ni wakati sasa wa mataifa ya Afrika, kutumia rasilimali zake kwa njia inayostahili na kuhakikisha kuwa kuna uadilifu kwenye utumizi wa fedha za serikali.

