NAIBU WA RAIS PROFESA KITHURE KINDIKI AMSUTA MTANGULIZI WAKE RIGATHI GACHAGWA.

Jukumu kuu la rais William Ruto sio kuongoza taifa la Kenya kwa mihula miwili.

Ni kauli ya naibu wa Rais Profesa Kithure Kindiki, ambaye amemsuta aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa, kutokana na kauli yake ya kuungana na viongozi wanaopinga uongozi wa Serikali ya Kenya kwanza, ili kuhakikisha kuwa Ruto hachukui hatamu ya uongozi kwa muhula mwingine wa pili.

Kwa mujibu wa Kindiki, malengo ya kiongozi wa taifa kwa sasa, ni kuhakikisha kuwa anatimiza ajenda ya kuboresha maisha ya wakenya, kupitia maendeleo kwenye jamii.

Wakati uo huo Kindiki ameelezea kuwa ataunga mkono utendakazi wa Rais William Ruto, ili kuhakikisha kuwa anafanikisha malengo yake kwa wakenya.