Taifa la Kenya linatarajiwa kubadilisha makadirio ya bajeti yake katika siku za usoni, ili kuziba mianya kwenye wizara ya afya, ambayo huenda ikashuhudiwa baada ya Marekani, kubadilisha sheria zake za ufadhili wa mataifa ya Afrika.
Kulingana na katibu anaye husika na masuala ya matibabu katika wizara ya afya nchini Harry Kimtai, tayari serikali kuu imeanzisha mikakati ya kuongeza mgao huo, ili kufanikisha huduma muhimu za matibabu kwa wananchi.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari humu nchini, Kimtai ameelezea kuwa, serikali itaangazia vitengo muhimu ziadi kwenye wizara hiyo, vitakavyo hitaji fedha za haraka ili kuendelezwa.
Wakati uo huo Katibu Kimtai ametaja suala la serikali kuu, kuwekeza zaidi katika kufadhili juhudi za kukabiliana maradhi kama vile, Malaria, Ukimwi na TB.

