Mabingwa mara ishirini na moja wa Ligi Huku hapa Nchini Gormahia, wapo kwenye Harakati za mwisho za kumsajili mshambuliaji wa Uganda Charles Bbaale Dirisha la uhamisho litakapofunguliwa siku ya Ijumaa, wakipania kuimarisha kikosi chao Bbaale akitamatisha mkataba wake wa misimu miwili na vigogo wa Rwanda Rayon Sports.
Mshambuliaji Huyo alijiunga na Rayon Sports mwaka Juzi baada ya kukipiga na Timu ya Nyumbani SC Villa, akiisadia Klabu Hio yenye makazi yake Kigali kunyakua Taji la Rwanda Super Cup, alipofunga goli Moja kwenye Ushindi wa Magoli matatu Sufuri dhidi ya APR FC.
Bbale ambaye tayari yupo nchini kwa mazungumzo na Kogalo, amekua na muda mchache kiwanjani Msimu huu akiliona lango mara mbili pekee, na iwapo atafanikiwa kusajiliwa na miamba hao wa hapa nchini, basi atajiunga na Mganda mwenzake Pius Akena kambini Humo.
Gormahia ambao wamekua wakisua sua kuandikisha matokeo bora msimu huu, hivi sasa wanashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu hapa nchini na alama ishirini na nane baada ya mechi Kumi na saba, alama nane nyuma ya viongozi Kenya Police, wataekena Miadi na Posta Rangers Siku Ya Jumamosi Huko Machakos.

