Idadi kubwa ya wakaazi wa eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi wameendelea kukabiliwa na changamoto kuu, katika kupata vitambulisho kutokana na hatua ya wao, kutakiwa kulipia stakabadhi hizo muhimu.
Akithibitisha hilo afisa anayehusika na sahihi za vidole katika afisi hiyo Ruth Hasango, ametaja suala la wananchi wengi kususia shughuli za kupata huduma hizo, kusababishwa na changamato za kifedha, zinazo wakabili kwenye jamii.
Akizungumza na mwanahabari wetu katika afisi ya vitambulisho hapa mjini Malindi, Hasango amesema kuwa huenda idadi ya wakenya wanaosajiliwa kupata vitambulisho vya kitaifa eneo hili, ikaongezeka hata zaidi, iwapo serikali itatupilia mbali ada za kupata vitambulisho.
Ni kauli ambayo imengwa mkono na mmoja wa wananchi katika eneo hili la Malindi kaunti ya Kilifi, Elias Mwalimu Karisa ambaye amesema kuwa kuwepo kwa ada hizo, kumewasababishia changamoto kuu hasa wakati wanapo poteza stakabadhi hizo muhimu.

