TIMO WERNER KUKOSA KOMBE LA DUNIA

Fowadi wa zamani wa klabu ya Chelsea Timo Werner ambaye sasa anachezea klabu ya Rb Leipzig atakosekana katika mashindano ya kombe la dunia mwaka huu yatakayofanyika nchini Qatar tarehe 20 mwezi November 2022.

Timo Werner mwenye umri wa miaka 26 atakosekana kwenye kipute cha mwaka huu baada ya kupata jeraha la mguu na klabu yake ya RB Leipzig ilitoa taarifa hiyo rasmi hapo jana.

Werner ameifungia timu yake ya taifa ya ujerumani mabao 24 katika mechi 55 za kitaifa ambazo ameshiriki mpaka kufikia sasa zikiwemo zile za kufuzu kwa kombe la dunia.

Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya ujerumani amemtakia afueni ya haraka mchezaji huyo ambaye msimu huu kunako ligi kuu ya ujerumani, amefunga mabao 9 baada ya kuagana na Chelsea klabu ambayo alikuwa na kipindi kibovu ndani ya msimu mmoja.