GERRARD PIQUE ASTAAFU SOKA RASMI

Mshindi wa kombe la dunia mwaka 2010 mwite Gerrard Pique na timu yake ya taifa ya Uhispania ni nguli atakayekosekana katika mashindano ya dunia mwaka huu baada ya kutangaza rasmi hapo jana kwamba mechi ya laliga ya wikendi hii ambapo klabu yake ya Barcelona itakuwa inavaana na Almeria itakuwa mechi yake ya mwisho kusakata soka la ushindani.

Pique ambaye alitangaza kustafu kupitia mtandao wake wa twitter ameshinda mataji manane ya laliga akiwa na uzi wa Barcelona, mataji saba ya copa del rey, mataji matatu ya uefa champions league katika mechi 600 alizochezea Barcelona.