SENETA WA TANA RIVER AWASHINIKIZA WENYEJI KUJIHUSISHA NA KILIMO

Seneta wa Tana River, Danson Mungatana amewashinikiza wakaazi wa kaunti hiyo kujihusisha na kilimo wakati huu kunaposhuhudiwa mvua kwa minajili ya kuimarisha uzalishaji wa chakula.
Akiongea na wanahabari, Mungatana amesema chakula kilichotolewa na serikali kuu hakitoshi na kwamba serikali inapanga kutatua swala la baa la njaa kwa kuweka fedha za kutosha kufanikisha kilimo nyunyizi
Mungatana amefichua kuwa tayari kaunti ya Tanariver imepokea mgao wa fedha kupitia afisi ya gavana baada ya wawakilishi wadi kupitisha bajeti hiyo huku akisema kuwa bado mahakama haijatoa tathmini ya kina itakayotoa mwelekeo kuhusu hazina ya ustawishaji maeneo bunge CDF