SS ASSAD KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA KAUNTI YA KWALE MICHEZONI

Klabu ya SS Assad ya kaunti ya kwale inayoshiriki katika ligi ya kitaifa ya Super League imetangaza kuwa inalenga kushirikiana na viongozi wa serikali ya kaunti hiyo kwenye kuimarisha talanta za vijana mashinani.

Katika mradi wa kuiendeleza SS Asad taarifa zasema kuwa takriban kima cha milioni 15 kitatumika kwenye kuutekeleza bila kukwama kauli ambayo imetolewa na rais wa klabu hiyo Richard Onsongo.

Serikali ya kaunti hiyo ikiongozwa na Fatuma achani imethibitisha utayari wa kushirikiana na klabu hiyo katika muradi wa makuzi ya talanta za vijana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *