Beki kinda raia wa Kenya Amos Wanjala aliyekuwa Kati ya wachezaji waliosajiliwa na klabu ya nastic soccer academy Uhispania kwa mafunzo ya kuimarisha soka lake sasa ni rasmi amejiunga na klabu ya Atletic Club Torrellano klabu inayoshiriki katika ligi ya daraja la tano nchini humo.
Wanjala ni Kati ya wachezaji waliokuwa kwenye kikosi cha Kenya cha U18 Juniors Stars kilichofika fainali kwenye mashindano ya Cecafa makala yaliyopita.
Wanjala alisajiliwa na Nastic Soccer Academy sawa na Aldrine Kibet pamoja na Allan Kasavuli.
Aldrine Kibet ambaye ni nahodha wa zamani wa timu ya shule ya upili ya St Anthony Kitale taarifa zasema kuwa anapendelea kupata usajili katika akademi ya Barcelona La Masia, sehemu aliyokulia Lionel Messi pamoja na masogora kama Andreas Iniesta, Xavi Hernandez pamoja na makinda wapya kama Dani Olmo, Lamine Yamal na kadhalika.