Bingwa wa Dunia katika mbio za mita 800 Mary Moraa amevunja rekodi ya mwanariadha Caster Semenya katika mbio za mita 600 usiku wa kuamkia leo huko Berlin.
Moraa alitumia muda wa dakika 1.21.63 na kuvunja rekodi ya semenya mzawa wa Afrika kusini ambaye alikuwa ameweka rekodi ya dakika 1.21.77 mwaka 2017 huko Ujerumani.
Ikumbukwe kuwa Moraa mwanzo wa msimu huu alitangaza kuwa analenga kuvunja rekodi zilizowekwa na watangulizi wake jambo ambalo ashalifanya kufikia sasa katika mbio hizo za mita 600