Huenda mkufunzi mwaduka Bakari akajiondoa katika klabu ya Bumbani stars kutoka kaunti ya kwale, klabu itakayoshirkki ligi ya Fkf daraja la Kwanza kitaifa msimu ujao.
Taarifa zasema kuwa Mwaduka amejiondoa katika klabu hiyo kwa kile kinachotajwa kuwa amekosewa heshima na uongozi wa klabu kuhusu mandalizi ya msimu mpya.
Kwenye taarifa za kuaminika ambazo mhusika aliyezungumza na Tama la SPOTI alitaka jina lake libanwe kwa sasa hadi tamati mwa mchakato huu ni kuwa klabu ya Bumbani Stars inalenga kuajiri mkufunzi mpya kutoka atakaye iongoza Bumbani msimu ujao jambo ambalo lilimkwaza Bakari.
Ikumbukwe kuwa Bakari ndiye mkufunzi aliyeisaidia klabu hiyo kutoka ligi za mashinani na kuipandisha daraja mpaka ligi ya daraja la kwanza kitaifa msimu uliopita kwa kushinda bingwa wa daraja la pili.